test

JAMII SI MTAZAMAJI WA UHALIFU BALI NI MSHIRIKI MKUU WA KUUZUIA" SACP MAKARANI

 

Babati. Manyara


Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limeitaka jamii mkoani humo kuendelea kufichuwa viashiria vya Uhalifu na watu wenye mienendo ya kutiliwa shaka ili wachukuliwe hatua   kwani jamii sio mtazamaji wa uhalifu bali ni mshiriki muhimu sana katika kuubaini, kuuzuia na kuutanzua katika jamii



Wito huo wa Ushirikishwaji jamii umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ahmed Makarani ofisini kwake wakati akielezea namna  Ushirikishwaji jamii unavyozuia uhalifu na wahalifu Mkoani hapa


" Ushirikiano kati ya jamii na Polisi ni nguzo muhimu ya amani na usalama. Bila ushirikiano huo, kudhibiti uhalifu huwa vigumu" amesema Makarani


Itakumbukwa kuwa   jamii kushirikiana na polisi

Kutapunguza uhalifu kwa 

Jamii kutoa taarifa mapema kuhusu wahalifu au vitendo vinavyotia shaka na polisi huchukua hatua kabla ya  madhara kutokea


SACP Makarani amesema Ushirikiano wa Polisi na Jamii kunaimarisha amani na utulivu katika jamii na kutoa fursa ya jamii kujishughulisha katika shughuli za kiuchumi na kijamii kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla


Ifahamike kwamba Jamii yeyote  salama hujengwa kwa ushirikiano, mawasiliano na uaminifu kati ya wananchi na polisi. 


"Polisi bila jamii hawawezi kufanikiwa, na jamii bila polisi haiwezi kuwa salama" Amesisitiza Makarani

JAMII SI MTAZAMAJI WA UHALIFU BALI NI MSHIRIKI MKUU WA KUUZUIA" SACP MAKARANI JAMII SI MTAZAMAJI WA UHALIFU BALI NI MSHIRIKI MKUU WA KUUZUIA" SACP MAKARANI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on February 04, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.