test

VALENTINE HII CHAGUA UPENDO,CHAGUA USALAMA BARABARANI, DTO BABATI.

 


Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, katika kusherehekea siku ya Valentine Februari 14, 2026, limegawa zawadi za Valentine na  kuwataka madereva wa vyombo vya moto wilayani hapa kuonesha upendo kwa abiria na watumiaji wengine wa Barabara kwa kuzingatia na kufuata sheria za Usalama Barabarani ili kukinga na ajali zinazoweza kuepukika


Wito huo umetolewa na Mrakibu wa Polisi (SP) Emmanuel Kandola na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Babati (DTO) Mkoa wa Manyara akiwa ameambatana na Sajenti wa Polisi Veronica pamona na  SGT  Isaya kutoka kikosi cha Usalama Barabarani  ambapo  amewataka madereva kuadhimisha siku ya Valentine kwa kuonyesha upendo  abiria wao kwa kuendesha kwa uangalifu vyombo vyao vya moto  kwa lengo la kupunguza ajali na  kulinda Maisha pamoja na  kujenga jamii salama


"Valentine hii chagua upendo, chagua Usalama Barabarani, Mpendwa wako anakusubiri urudi salama" amemalizia DTO SP Kandola

VALENTINE HII CHAGUA UPENDO,CHAGUA USALAMA BARABARANI, DTO BABATI. VALENTINE HII CHAGUA  UPENDO,CHAGUA USALAMA BARABARANI, DTO BABATI. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on February 15, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.