test

WALIMU WALIOFAULISHA KIDATO CHA NNE 99.8% BABATI DC WAPONGEZWA

 Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe Emmanuela Kaganda amewapongeza walimu wote waliofundisha kidato cha Nne  katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mpaka kufahulisha Kwa asilimia 99.8. kwa mwaka 2025. Mhe Kaganda ameyasema hayo leo kwenye Hafla ya kuwapongeza walimu wote waliofundisha kidato cha Nne kwa mwaka  2025 iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ayalagaya Sekondari.  "Tunashukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa kuboresha  mazingira ya kufundisha na kufundishia yaliyopelekea shule nyingi za Halmashauri ya Wilaya Babati  kufanya vizuri ' amesisitiza kiongozi huyo. Mhe Kaganda ameagiza Wakuu wa Shule kulinda na kutunza  miundombinu ya shule hizo akasisitiza kila mwisho wa mwaka mara baada ya kidato cha nne kumaliza Madarasa hayo kupakwa rangi kwa kushirikiana na wazazi.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewapongeza Walimu hao kwa kazi nzuri waliofanya kwa mwaka 2025 akiwasihi wasibweteke na matokeo yaliyopatikana bali waongeze bidii za ufundishaji na malezi .Mkurugenzi Mbogo amesisitiza Kila shule kuweka Maandalizi mapema ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2028 . Aidha Mkurugenzi Mbogo ameshukuru Naibu Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Babati Vijiji  Mhe Daniel Sillo kwa mchango wake wa mkubwa wa kuboresha Elimu. 

Wakati huo huo Mkurugenzi Mbogo amewashukuru Wadau wa Maendeleo wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kuwa chachu katika matokeo ya mwaka 2025. Hafla ya kuwapongeza walimu waliofundisha kidato cha Nne 2025 imeenda sambamba na utoaji wa zawadi kwa shule zote na imehudhuliwa na Viongozi mbalimbali Kutoka Mkoani na Wilaya ya Babati

WALIMU WALIOFAULISHA KIDATO CHA NNE 99.8% BABATI DC WAPONGEZWA WALIMU WALIOFAULISHA KIDATO CHA NNE 99.8%  BABATI DC WAPONGEZWA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on February 16, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.