test

ASKOFU LAGWEN: MAANDIKO MATAKATIFU NI LISHE YA KIROHO

 

Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu, Anthony Lagwen, amewataka waumini kujenga tabia ya kusoma Maandiko Matakatifu akisisitiza kuwa ndiyo lishe muhimu ya kiroho inayosaidia kuimarisha imani.



Askofu Lagwen ametoa wito huo wakati wa adhimisho la Misa Takatifu ya Alhamisi Kuu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Agustino Katesh wilayani Hanang mkoani Manyara.


Amesema pamoja na kusoma neno la Mungu, waumini wanapaswa kujitahidi kupokea sakramenti mara kwa mara ili kuimarisha uhusiano wao na Mungu.


Aidha, amewahimiza waumini kuanza na kudumisha maisha ya sala, wakimwomba Mungu awe pamoja nao katika kila hatua ya maisha yao ya kila siku.


Katika mahubiri yake, Askofu Lagwen alisisitiza umuhimu wa waumini kujidhatiti katika imani na kutenda haki kwa watu wote bila ubaguzi, akieleza kuwa huo ndio msingi wa maisha ya Kikristo yenye kumpendeza Mungu.





Misa hiyo ya Alhamisi Kuu imehudhuriwa na mamia ya waumini waliokusanyika kushiriki ibada hiyo muhimu katika kalenda ya Kanisa. 


ASKOFU LAGWEN: MAANDIKO MATAKATIFU NI LISHE YA KIROHO ASKOFU LAGWEN: MAANDIKO MATAKATIFU NI LISHE YA KIROHO Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on April 03, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.