Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amekanusha vikali taarifa zilizosambaa zikidai kuwa mwanaume mmoja katika eneo la Kimara alichukuliwa sehemu zake za siri.
Akizungumza na vyombo vya habari, Muliro amesema tukio hilo halina ukweli wowote na ni uzushi uliobuniwa kwa lengo la kuzua taharuki na hofu kwa wananchi. Akiongeza kuwa uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kuwa aliyesema ameibiwa nyeti zake alikutwa nazo baada ya kukaguliwa.
Aidha Jeshi la Polisi, limewataka wananchi kupuuza taarifa hizo na kuacha kusambaza uvumi usio na uthibitisho, huku likisisitiza umuhimu wa kupata taarifa kutoka vyanzo rasmi ili kuepuka taharuki zisizo za lazima.
Aidha, amewahimiza wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pale wanapokutana na matukio ya uhalifu badala ya kusambaza habari zisizo na uhakika mitandaoni.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
April 04, 2026
Rating:

No comments: