Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Emmanuel Gekul ametoa miche 25,000 ya miti ya vivuli, matunda pamoja na mbao kwa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Babati Vijijini ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira na mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira.
Tangazo la utoaji wa miche hiyo lilitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Manyara Jannes Darabe wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Kimkoa yaliyofanyika hivi karibuni katika Kata ya Ufana, wilayani Babati mkoani Manyara, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Viti Maalum Tanzania Bara kupitia Jumuiya ya Wazazi, Catherine Canute Joachim.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Dkt. Catherine Joachim amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kulinda vyanzo vya maji.
“Tunahitaji jamii inayojali mazingira kwa vitendo. Kupanda miti ni uwekezaji mkubwa kwa kizazi cha sasa na kijacho,” alisema Dkt. Catherine.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
May 19, 2026
Rating:


No comments: