wa Makanisa Mkoa wa Arusha,Kilimanjaro na Manyara na Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, Stanley Hotay amesema Taifa la Tanzania linahitaji msamaha ili kuponya majeraha yanayotokana na tofauti za kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Hotay, amemtembelea Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Bunge jijini Dodoma.
Askofu Hotay alikuwa ameambatana na baadhi ya wachungaji kutoka dayosisi hiyo, ambapo walifanya mazungumzo mbalimbali yaliyolenga kuimarisha ushirikiano na kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya jamii.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wa dini walisisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha amani, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania kwa ajili ya kujenga taifa lenye maendeleo na ustawi.
Aidha, wameeleza kuwa amani ni msingi muhimu wa maendeleo katika nyanja mbalimbali, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuilinda na kuendelea kuhamasisha umoja na maelewano katika jamii.
Ziara hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya viongozi wa dini na viongozi wa serikali katika kuendeleza masuala yenye maslahi mapana kwa wananchi.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
June 18, 2026
Rating:


No comments: