test

DC SEMINDU AHAMASISHA WANANCHI WA MBULU KUJITOKEZA KWA WINGI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU 2026

 

Wananchi wa Wilaya ya Mbulu wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shughuli za mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, zitakazofanyika Julai 16, 2026 katika Viwanja vya Tsorii, Kata ya Gehandu.



Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Michael Semindu, leo Juni 16, 2026, wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotarajiwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu.


Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Semindu alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ni mali ya Watanzania wote, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shughuli za mapokezi na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi.




“Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa Julai 16, 2026 katika Viwanja vya Tsorii, Kata ya Gehandu. Baada ya hapo, utakimbizwa katika maeneo mbalimbali ambapo utatembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma kwa wananchi,” alisema Mhe. Semindu.


Aidha, aliwataka wananchi kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano, akieleza kuwa Mwenge wa Uhuru ni chombo muhimu cha kuhamasisha maendeleo na kuimarisha uzalendo miongoni mwa Watanzania.


Kwa upande wao, wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu wamesema kuwa wako tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru 2026, wakibainisha kuwa ni alama ya amani, umoja na maendeleo ya Taifa. Hivyo, watajitokeza kwa wingi kushiriki katika shughuli zote zinazohusiana na mapokezi yake.


Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru 2026: “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo.”



DC SEMINDU AHAMASISHA WANANCHI WA MBULU KUJITOKEZA KWA WINGI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU 2026 DC SEMINDU AHAMASISHA WANANCHI WA MBULU KUJITOKEZA KWA WINGI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU 2026 Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on June 18, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.