test

LUNGU KUZIKWA JUNI 29.2026

 Baada ya kukaa mochari kwa zaidi ya mwaka mmoja hatimaye mwili wa Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu utazikwa huko Waterkloof Ridge, Pretoria, Afrika Kusini, tarehe 29 Juni 2026. Familia ya Rais Lungu imeshinda kesi na kumaliza mvutano wa zaidi ya mwaka mmoja wa mahakamani kuhusu hatima ya mazishi ya kiongozi huyo.



Awali Serikali ya Zambia ilitaka Rais Lungu azikwe huko Embassy Park, Lusaka, eneo lililotengwa rasmi kwa mazishi ya viongozi wakuu wa kitaifa lakini familia ilipinga uamuzi huo kutokana na uhasama uliokuwepo kati ya Rais Lungu na Rais wa sasa Hakainde Hichilema.


Wakati Lungu akiwa madarakani aliwahi kumshtaki Hichilema kwa makosa ya UHAINI wakati Hichilema akiwa kiongozi wa upinzani. Baada ya kusota gerezani hatimaye Hichilema alitoka na kugombea urais mwaka 2021 na kumshinda Lungu, hali iliyoongeza mzozo baina yao.


Baada ya Lungu kufariki Juni 05, 2025, akiwa anapatiwa matibabu ya saratani ya umio (oesophageal cancer) huko Pretoria familia ilitaka azikwe Afrika Kusini, lakini serikali ilitaka azikwe Zambia.


Familia ikiongozwa na mke wa marehemu, Bi.Ester Lungu ilisema marehemu aliacha wosia kwamba akifa asizikwe Zambia na viongozi wote wa serikali wakiongozwa na Rais Hichilema wasihudhurie mazishi yake. Familia ilitumia wosia huo kupinga serikali kuandaa mazishi ya Lungu.


Serikali ya Zambia ilifungua kesi katika Mahakama Kuu ya Gauteng na hukumu ilipotoka June 23, 2025 mahakama hiyo iliipa serikali ya Zambia haki ya kumzika Lungu kwa mazishi ya kitaifa. Hata hivyo familia ilikata rufaa Mahakama ya Rufani (Supreme Court of Appeal), iliyopo Bloemfontein, kupinga uamuzi wa Mahakama ya Gauteng.


Hatimaye jana Juni 23, 2026 Jaji R.M. Keightley amebatilisha uamuzi wa Mahakama kuu ya Gauteng, uliokuwa umeipa serikali ya Zambia haki ya kurejesha mwili kwa mazishi ya kitaifa. Hukumu hii ni ya mwisho na serikali ya Zambia haiwezi kukata rufaa popote. Kufuatia maamuzi hayo Edgar Lungu atakuwa rais wa kwanza wa Zambia kuzikwa nje ya nchi.!



LUNGU KUZIKWA JUNI 29.2026 LUNGU KUZIKWA JUNI 29.2026 Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on June 24, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.