Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Dr Emmanuel Nuwas amesema daraja la eneo la Endahagichan ambalo lilikuwa kero kubwa kwa wananchi kutokana na kukwamisha mawasiliano na shughuli za kijamii na kiuchumi, sasa limekamilika na kuanza kutumika rasmi.
Dr Nuwas amesema kukamilika kwa daraja hilo ni utekelezaji wa ahadi aliyowapa wananchi wakati wa kampeni, ambapo walimuomba kusaidia kumalizia ujenzi wa daraja hilo lililokuwa limekwama kwa muda mrefu.
“Kazi tayari Endahagichan, sasa mwendo ni kwa kwenda mbele. Tumekamilisha daraja lililokwama na liko tayari linatumika. Nakumbuka tulipelekwa hapo wakati wa kampeni kwamba ninawaahidi nini kuhusu kumalizia daraja hili, sasa kazi imekamilika,” amesema Dr Nuwas.
Amesema wananchi wa maeneo hayo walikuwa wakikumbana na changamoto za usafiri na mawasiliano hasa kipindi cha mvua, hali iliyokuwa ikiathiri shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mbunge huyo amesema ataendelea kutekeleza ahadi zake hatua kwa hatua kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo na kuboresha huduma katika jimbo hilo.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
June 07, 2026
Rating:



No comments: