test

WALIMU 540 WA MANISPAA YA ILEMELA WATUNUKIWA VYETI VYA PONGEZI

 

Jumla ya walimu 540 wa shule za msingi na sekondari wa Manispaa ya Ilemela wametunukiwa vyeti vya pongezi kufuatia kazi nzuri na yenye weledi wanayofanya iliyopelekea Ilemela kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kwa ngazi zote msingi na sekondari kwa takribani miaka minne mfululizo.



Tuzo hizo za pongezi zimekabidhiwa tarehe 06 Juni 2026b kupitia tamasha la Ilemela mwalimu festival lililoambatana na kauli mbiu isemayo Elimu bora huanzia kwa mwalimu aliethaminiwa ikiwa ni sehemu ya kuwaongezea hamasa katika kufanya kazi.




Akizungumza katika tamasha hilo mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda  amesema mkoa wa Mwanza umekua kinara kwenye matokeo ya kitaifa ya shule ya msingi na sekondari kwa miaka mingi sababu ya juhudi na kazi nzuri wanazofanya walimu hivyo ni budi kuwapongeza na kuwataka kuendelea kuwa walezi wazuri wa watoto kimasomo na kimaadili na ameahidi kuwa serikali itaendelea kutatua changamoto zao kadili itakavyopata nafasi.


“Matokeo ya kidato cha pili sasa tumefikia asilimia tisini (90%), kidato cha nne 99% na darasa la saba 92%, kazi hiyo bora na yakutukuka inafanywa na nyie walimu na mafanikio ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hayawezi kutenganishwa na jitihada zenu kubwa mnazofanya” Alisema RC Mtanda.


Aidha Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Amiri Mkalipa, amesema dhamira ya serikali ya kuwakutanisha pamoja walimu wote wa shule za serikali na binafsi ni kutambua jitihada wanazofanya na kuwapongeza mafanikio wanayoyaleta Ilemela kwa kuongoza kwa ufaulu wa wanafunzi kimkoa na hata kitaifa.  




Naye Bi.Ummy Wayayu, mkurugenzi wa manispaa amesema mafanikio ya kielimu yaliyopo Ilemela ni jitihada za serikali kwa kuweka mazingira bora na wezeshi ya kufundisha na ujifunzaji kwa wanafunzi pamoja na ushirikiano mzuri wa viongozi na walimu katika utendaji kazi na utatuzi wa changamoto zote zote za elimu.


Mwl. Emmanuel Reuben kutoka shule ya sekondari Mihama na Mwl.Zubeda Mwangu Hamis kutoka shule ya msingi Gedeli  wamesema wamefurahishwa sana na tamasha kwani limewapa hamasa katika utendaji kazi wao kwa juhudi zao kutambuliwa na kupewa thamani na wameomba jambo hili liwe

WALIMU 540 WA MANISPAA YA ILEMELA WATUNUKIWA VYETI VYA PONGEZI WALIMU 540 WA MANISPAA YA ILEMELA WATUNUKIWA VYETI VYA PONGEZI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on June 07, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.