test

MHE RGINA NDAEGE AZIKUMBUKA SHULE,ZAHANATI NA VITUO VYA AFYA BABATI DC.

 Naibu Waziri Ofisi ya  Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Regina Ndege Qwaray ametoa  viti,45  kompyuta/ laptop 36 kabati, na meza  kwa shule za msingi  Sekondari,  zahanati na vituo vya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati



Akizungumza kwenye Hafla fupi ya ugawaji vifaa hivyo leo katika Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe Qwaray amesema vifaa hivyo amevipata kutoka kwenye Taasisi mbalimbali na kuona uhitaji katika shule , zahanati , vituo vya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati.



Wakati huo huo Mhe Qwaray amepata fursa ya kuongea na Watumishi ambapo amewapongeza Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kujituma kufanya kazi na kutatua changamoto za Wananchi. 


Aidha Mhe Qwaray amesisitiza Watumishi hao kujenga mahusiano  mazuri kati yao na Watumishi wengine na wananchi ujumla ili kujiletea maendeleo huku  akisisitiza Watumishi kuithamini na kupenda  kufanya kazi. 



Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe John Noya na Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo wameshukuru kwa msaada huo na kuomba  ushirikiano huo uendelee.

MHE RGINA NDAEGE AZIKUMBUKA SHULE,ZAHANATI NA VITUO VYA AFYA BABATI DC. MHE RGINA NDAEGE AZIKUMBUKA SHULE,ZAHANATI NA VITUO VYA AFYA BABATI DC. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on June 12, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.