test

DCEA yazindua Filamu ya Kifurushi kuimarisha mapambano dhidi ya usafirishaji wa dawa za kulevya nchini



MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imezindua rasmi filamu maalumu ya elimu ijulikanayo kama “Kifurushi” yenye lengo la kuongeza uelewa wa jamii kuhusu mbinu zinazotumiwa kusafirisha dawa za kulevya kupitia vyombo vya usafiri wa umma na kuwatahadharisha wananchi dhidi ya kubeba mizigo au vifurushi wasivyovifahamu.



Uzinduzi huo umefanyika Juni 12, 2026 katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam, ukiongozwa na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas James Lyimo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya usafirishaji, wasanii,waigizaji na taasisi zinazoshiriki katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kamishna Jenerali Lyimo amesema,dawa za kulevya zinaendelea kuwa tishio kubwa kwa afya za wananchi, ustawi wa familia, usalama wa jamii na maendeleo ya taifa kutokana na madhara yake makubwa ya kijamii na kiuchumi.




Amesema,matumizi na biashara ya dawa za kulevya huchangia kuongezeka kwa uhalifu, kuvunjika kwa familia, kudhoofika kwa nguvu kazi ya taifa na kupungua kwa tija katika shughuli za uzalishaji mali, hususan miongoni mwa vijana ambao ndio nguvu kazi muhimu ya taifa.


“Dawa za kulevya si tatizo la mtu mmoja mmoja bali ni changamoto ya taifa zima. Athari zake zinaigusa jamii kwa ujumla na kuathiri maendeleo ya nchi katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi,”amesema Kamishna Jenerali Lyimo.


Amebainisha kuwa,Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo kupitia operesheni za ukamataji, uchunguzi wa makosa ya dawa za kulevya, utoaji wa tiba kwa waathirika pamoja na kampeni za elimu kwa umma.


Kwa mujibu wa Lyimo, uchunguzi unaofanywa na mamlaka hiyo umebaini kuwa wahalifu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya wamekuwa wakibuni mbinu mpya za kuzisafirisha, ikiwemo kuzificha katika mizigo na vifurushi vinavyoonekana kuwa vya kawaida.


Amesema,baadhi ya wananchi wamejikuta wakikabiliwa na mkono wa sheria baada ya kukubali kubeba mizigo wasi...

DCEA yazindua Filamu ya Kifurushi kuimarisha mapambano dhidi ya usafirishaji wa dawa za kulevya nchini  DCEA yazindua Filamu ya Kifurushi kuimarisha mapambano dhidi ya usafirishaji wa dawa za kulevya nchini Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on June 12, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.