test

SMAUJATA KANDA YA KASKAZINI WAFANYA ZIARA MESERANI ARUSHA

 

Jumuiya ya Smaujata Kanda ya Kaskazini imefanya ziara ya utaliii na utamaduni MESERANI PARK Mkoani Arusha Kwa lengo la kujifunza na  kutangaza utalii wa ndani kuunga mkono Royal tower aliyoianzisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Akizungumza kwa niaba ya Smaujata Kanda ya Kaskazini Shujaa Ezekiel Tlanka katibu wa Smaujata Kanda ya Kaskazini alisema tumefurahia utalii huu wa ndani maana ni mzuri sana hivyo tukitoka hapa kama Jumuiya ya Smaujata Kanda ya Kaskazini tunaenda kutangaza Ili Kila mtanzania aende kujionea mazuri hayo.


Awali Jumuiya ya Smaujata Kupitia Idara yake ya Makongamano na utalii Smaujata Taifa walielekeza Kila Kanda ikafanye utalii wa ndani ambapo Kanda ya Kaskazini ilifanya Meserani Mkoani Arusha.


Jumuiya ya Smaujata walipokekewa na uongozi wa Meserani na walianza kutembelea mabanda ya nyoka kujifunza aina za nyoka wakali na wasiowakali na Kila aina ya ndege kwa kweli wafurahia. Walijifunza utamaduni wa kimasai na walivaa mavazi ya kiutamaduni wa wamasai .


Smaujata Kanda ya Kaskazini imemshukuru Mhe. Rais pamoja na serikali yake ya awamu ya sita kwa kuendelea kulinda sekta ya utalii Tanzania .


Imeandaliwa na idara ya habari na mawasiliano Kanda ya Kaskazini

SMAUJATA KANDA YA KASKAZINI WAFANYA ZIARA MESERANI ARUSHA SMAUJATA KANDA YA KASKAZINI WAFANYA ZIARA MESERANI ARUSHA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on June 30, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.