Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Rahma Musa Tito (16), mkazi wa Kijiji cha Msoga, Wilaya ya Chalinze, kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi, Hadija Hemedi Shaha (51), aliyekuwa mkulima na mwenye ulemavu wa miguu yote miwili.
Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo lilitokea usiku wa Julai 28, 2026, ambapo mtuhumiwa anadaiwa kumshambulia mama yake na kumchoma kichwani kwa kutumia kitu chenye ncha kali, baada ya kuzuiwa kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa (Birthday Party) ya rafiki yake iliyokuwa ikifanyika karibu na Hospitali ya Msoga.
Mwili wa marehemu uligunduliwa asubuhi ya Julai 29, 2026 na fundi ujenzi aliyefika nyumbani hapo kufuata mfuko wa saruji na malipo yake. Baada ya kufunguliwa mlango na mtuhumiwa, alikuta mwili wa marehemu ukiwa umelala sakafuni na majeraha kichwani yaliyokuwa yakivuja damu.
Mwili wa marehemu ulipelekwa Hospitali ya Msoga kwa uchunguzi wa daktari kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika kutoka Jeshi la Polisi.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
July 30, 2026
Rating:

No comments: