test

MWANRI ATEULIWA KUWA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA

 Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kimefanya mabadiliko madogo ndani ya Sekretarieti ya chama hicho, yakihusisha uteuzi wa viongozi katika nafasi mbalimbali.



Katika mabadiliko hayo, Agrey Mwanri ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi ya John Mongella.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha Halmashauri Kuu iliyokutana  Visiwani Zanzibar Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Kihongosi amesema uteuzi huo ni sehemu ya maboresho ya Sekretarieti ya CCM yanayolenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya chama.


Sambamba na uteuzi wa Mwanri, Abdi Mahmud Abdi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar. 


Paul Chacha ameteuliwa kuongoza Idara ya Organizesheni akichukua nafasi ya Issa Ussi Gavu, huku Jamal Kassim akiteuliwa kuongoza Idara ya Uchumi kuchukua nafasi ya Raila Burhan Ngonzi.


Katika mabadiliko hayo, baadhi ya viongozi wameendelea kubaki katika nafasi zao, akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha-Rose Migiro, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, pamoja na Katibu wa NEC wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Hamid.

MWANRI ATEULIWA KUWA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA MWANRI ATEULIWA KUWA NAIBU KATIBU MKUU CCM  BARA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on July 29, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.