test

BABATI DC KUCHANJA WATOTO ZAIDI YA 128,000

 Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara inategemea kutoa chanjo ya polio kwa zaidi ya Watoto 128,000

kuanzia tarehe 27 hadi 30/8/2026.



Hayo yamesemwa leo na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Babati Dkt Hosea Madama kwenye kikao cha watu wenye



Ushawishi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, "Halmashauri yetu ni Mojawapo itayofanya zoezi la chanjo ya Polio kwa Watoto chini ya miaka 10 kuanzia trh 27 hadi 30.8.2026 na tunategemea kutoa chanjo kwa zaidi ya Watoto 128,000" amesisitiza Kiongozi huyo

Wakati huo huo Ndg Madama ameomba wajumbe wa kikao hicho ambao ni watu wenye ushawishi kwenye jamii kwenda kuhamasisha jamii kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hili

muhimu Kitaifa

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika kikao hicho ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg.Benedict Ntabagi amesema Chanjo ni Kinga hivyo

wananchi wenye Watoto chini ya miaka 10 ni lazima

wahamasishwe, waelimishwe na wajitokeze kwa wingi kupeleka Watoto wao kwenye chanjo ya Polio

Katika kikao hicho wananchi wamejulishwa kuwa chanjo ya polio ni nzuri, salama na imedhibitishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni ( WHO).

Wakiendelea na utoaji wa Elimu ya chanjo, wajumbe wa kikao hicho wameombwa kwenda kuhamasisha na kutoa umuhimu wa chanjo katika maeneo yao ili wananchi wapeleke Watoto wao ifikapo tarehe 27 hadi 30/8/2026

Kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi wa Dini, Mila, wazee maarufu, Makundi maalumu na watu wengine wenye ushawishi kwenye jamii ambao wameshukuru uongozi Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa ushirikishwaji huo na kuhaidi kwenda kutoa hamasa kwa wananchi katika maeneo yao juu ya umuhimu wa kushiriki katika zoezi la chanjo ya Polio.

BABATI DC KUCHANJA WATOTO ZAIDI YA 128,000 BABATI DC KUCHANJA WATOTO ZAIDI YA 128,000 Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on August 24, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.