test

MANYARA TANZANITE MARATHON YABAMBA MAMIA WAJITOKEZA.



Mamia ya wananchi na wanariadha kutoka maeneo mbalimbali wamejitokeza kushiriki Manyara Tanzanite Marathon iliyofanyika leo katika Mji wa Babati, mkoani Manyara.



Mbio hizo za hisani zimefanyika ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha jamii kuchangia ujenzi wa wodi maalum ya kuwahudumia watoto njiti, huku lengo likiwa ni kukusanya shilingi bilioni 1.5.


Zikiwa na kauli mbiu “Hatua Moja, Okoa Maisha ya Mtoto Njiti,” mbio hizo zimewakutanisha wananchi, wanariadha na wadau mbalimbali katika kuunga mkono juhudi za kuimarisha huduma kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.




Manyara Tanzanite Marathon imekuwa pia fursa ya kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za kijamii na kusaidia juhudi za kuokoa maisha ya watoto njiti mkoani Manyara.


#visionmedia Tz,updates #hatuamojaokoamaishayamtotonjiti

MANYARA TANZANITE MARATHON YABAMBA MAMIA WAJITOKEZA. MANYARA TANZANITE MARATHON YABAMBA MAMIA WAJITOKEZA. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on August 22, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.