test

BABATI DC YAZINDUA CHANJO YA POLIO KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 10

 Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara imezindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto chini ya Miaka 10 zoezi balo limeanza jana katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.






Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati, Remidius Mwema, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, amewataka wazazi na walezi kuitikia zoezi hilo kwa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya polio ili kuwalinda dhidi ya ugonjwa huo ambao unaweza kusababisha ulemavu.


Mwema amesisitiza umuhimu wa wazazi kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa afya wanaofika katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha watoto wote wanaostahili chanjo wanapata huduma hiyo.


Kwa upande wake, Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, James Mleli, amesema zaidi ya watoto 160,000 wanatarajiwa kufikiwa na chanjo ya polio katika halmashauri hiyo.


Amesema lengo ni kuhakikisha kila mtoto anayestahili anapata chanjo hiyo kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa polio.


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Anna Mbogo, amesema zoezi la utoaji wa chanjo linafanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyumba kwa nyumba, shuleni na maeneo ya mikusanyiko ya watu, ili kuwafikia watoto wengi zaidi.


Ameongeza kuwa wazazi na walezi wanapaswa kutumia fursa hiyo kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo kwa wakati.

BABATI DC YAZINDUA CHANJO YA POLIO KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 10 BABATI DC YAZINDUA CHANJO YA POLIO KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 10 Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on August 28, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.