Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini na NAIBU SPIKA wa BUNGE Mhe. Daniel sillo amefanikisha kumlipia BIMA ya Afya MTOTO Saumu Ally(12) mwenye ulemavu mkazi wa Kata ya kash majengo.
SILLO alikutana na Binti huyo mlemavu hivi karibuni Baada ya kufanya mkutano wa hadhara kash majengo na kuahidi kushughulikia BIMA ya Afya Kwa Binti huyo.
Akizungumza Kwa niaba ya familia mama mzazi wa Binti huyo, Hadija Issa Amemshukuru mhe Sillo Kwa msaada huo wa BIMA Kwa mwanae mwenye ulemavu.
Ameeleza kuwa Binti huyo tangu azaliwe hawezi kusimamia Wala kuongea jambo Lililo walazimu kumpeleka katika hospitali mbalimbali bila mafanikio yeyote, hivyo kupatikana Kwa BIMA Kwa Binti huyo itasaidia kuipunguza Gharama za matibabu walizo kuwa wakizitumia awali.
SILLO AFANIKISHA KUMLIPIA BIMA YA AFYA MTOTO SAUMU ALLY
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
August 27, 2026
Rating:
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
August 27, 2026
Rating:


No comments: