Upande wa Jamhuri umefunga rasmi ushahidi wake katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, baada ya kuwasilisha ushahidi kupitia mashahidi 17.
Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, ameieleza Mahakama Kuu kuwa baada ya kupitia ushahidi uliowasilishwa na ule uliobaki, upande wa mashtaka umeona kuwa ushahidi uliopo unatosheleza na hivyo umeamua kufunga kesi yake.
Jamhuri pia imeomba Mahakama iruhusu pande zote kufanya submissions kuhusu kama Lissu ana kesi ya kujibu (case to answer), hatua ambayo Lissu ameikubali.
Hata hivyo, Lissu amepinga hoja ya Serikali kwamba hakuna kifungu kinachozungumzia hatua hiyo, akirejea Kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), akisema baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi, Mahakama inapaswa kusikiliza hoja za pande zote kuhusu iwapo kuna kesi ya kujibu.
Lissu: “Kwa vile upande wa mashtaka umefunga ushahidi wao, hoja inayofuata ni Waheshimiwa Majaji kutusikiliza mimi na mawakili wa Serikali kuwaelezeni kwamba kuna kesi ya kujibu au la, ili tumalize mchezo hapa.”
Lissu ambaye anashikiliwa kwa takribani siku 495 gerezani anakabiliwa na shtaka la Uhaini ambalo kimsingi huku yake ni kifo kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
Alikamatwa mkoani Ruvuma muda mfupia baada ya kumaliza mkutano wa hadhara, Aprili 9,2025 na kusafirishwa hadi Dar es Salaam ambapo alipandishwa kwa mara ya kwanza Mahakama ya Kisutu Aprili 10, 2025 na kusomewa mashtaka ya Uhaini na Uchochezi
Kesi inaendele, endelea kutufatilia kwa taarifa zaidi
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
August 17, 2026
Rating:

No comments: