test

MASHINDANO YA STAN CUP FURSA KWA VIJANA MAGUGU

 

NAIBU WAZIRI waUtumishi na utawala Bora ambaye ni Mbunge wa viiti MAALUMU Mkoa WA MANYARA,amepongeza DIWANI wa Magugu mhe. Stanley Charles, Kwa ubunifu kuanzisha ligi katika Kata maarufu kama STAN CUP.



Mmhe Regina amesema DIWANI huyo ni mfano wa kuigwa Kwa kuanzisha jambo Hilo kubwa kwani  ni FURSA kubwa Kwa vijana wa Kata hiyo.


Katika Uzinduzi huo Mhe Regina anetumia FURSA hiyo kuwaasa vijanakutokujihusisha na uvunjifu wa AMANI ya NCHI Bali wajikite katika uzalishaji Mali.

Aidha mhe. Regina amekabidhi jumla ya jezi pea ishirini na mipira 20 kwaajili ya michuano hiyo ya Stan cup.


DIWANI wa Kata hiyo Mhe Stanley Charles amemshukuru mhe Regina Kwa moyo wa upendo Kwa Wana michezo wa Kata ya Magugu.




Amesema kuwa michuano hiyo itahusisha jumla ya TIMU 18 za Kata hiyo ambapo watakao fuzu vyema watapatiwa zawadi.


Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika Kwa miezi mitatu mfululizo katika viwanja mbali mbali vya Kata ya ya Magugu.

Katika Uzinduzi huo za wadi mbali mbali zilitolewa Kwa washindi wa michezo ya Baiskeli,Riadha na Bao. Ambao ilifanyika kabla ya Uzinduzi wa ligi.

MASHINDANO YA STAN CUP FURSA KWA VIJANA MAGUGU MASHINDANO YA STAN CUP FURSA KWA VIJANA MAGUGU Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on August 15, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.