test

MADIWANI MBULU WATAKA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA WAJASIRIAMALI UHAHARAKISHWE

 

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara wameiomba Serikali kuharakisha utoaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo ili waweze kutambulika rasmi na kurahisishiwa upatikanaji wa huduma mbalimbali katika taasisi za Serikali, ikiwemo mikopo yenye masharti nafuu ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.





Wakizungumza katika kikao cha robo ya nne cha mwaka wa fedha 2025/2026, madiwani hao wamesema kuchelewa kwa utoaji wa vitambulisho hivyo ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wajasiriamali wadogo na kusababisha baadhi yao kushindwa kupata mikopo kwa wakati.....





Naye Mbunge  wa Jimbo la  mbulu vijijini Emanuel Nuwas ameitaka Halmashauri kuhakikisha madiwani na viongozi wengine wanashirikishwa wakati wa utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali, ili kuwe na uwazi na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha hizo.....



Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii amesema Serikali kupitia halmashauri inaendelea kutoa elimu kwa wajasiriamali kuhusu taratibu na vigezo vya kunufaika na mikopo hiyo, huku akiwataka wajasiriamali kuhakikisha wanakamilisha mahitaji yanayotakiwa ili kurahisisha mchakato wa kupata mikopo.





MADIWANI MBULU WATAKA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA WAJASIRIAMALI UHAHARAKISHWE MADIWANI MBULU WATAKA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA WAJASIRIAMALI UHAHARAKISHWE Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on August 21, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.