test

WIZARA YA AFYA KUANZA KUTOA CHANJO YA POLIO YA MATONE.

 

Wizara ya Afya imetangaza kuanza kampeni ya chanjo ya Polio ya matone kwa Watoto chini ya miaka 10 kwa Mikoa 8 ya Tanzania bara kuanzia Agosti 27 hadi 30,2026 



Akizungumza katika semina kwa Waandishi wa habari na Maafisa Habari wa Halmashauri za Mkoa wa Manyara kuhusu chanjo hiyo, Dkt. Mwendwa Mwenesi ametaja Mikoa hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dodoma na Mara kwa Awamu hii ili kuhakikisha afya ya Watoto dhidi ya ugonjwa huo wa Polio.








Dkt Mwendwa amesema jumla ya Watoto 6,555,511 katika Mikoa hiyo itafikiwa wakiwemo Watoto 675,630 wa Mkoa wa Manyara.

 

Pia amesisitiza kuwa ugonjwa wa Polio ambao unasababishwa na virusi aina ya polio hauna tiba lakini unaweza kuzuiliwa kwa kupata chanjo ya polio ambayo hutolewa kwa njia ya matone (OPV) au Sindano (IPV). 


Hii ni kutokana na kubainika kwa uwepo  wa virusi vya polio katika mazingira hususani kwenye sampuli ya maji taka katika Mkoa wa Mwanza katika utafiti uliofanyika hivi karibuni. 


Vilevile ameongeza kuwa magonjwa mengine yanayoweza kuzuiliwa kwa njia ya chanjo ni pamoja kupooza, surua, Rubela, Pepopunda, Dondakoo, Kifaduro, Kifua kikuu, Kuhara pamoja na  kichocho. 


Dkt.Mwendwa ametaja dalili kuu za ugonjwa wa polio kuwa ni pamoja na kupooza/Ulemavu wa ghafla wa viungo ulio tepetepe, kulegea kwa viungo , kukosa nguvu,  kushindwa kunyanyua mguu au mkono ambako hakuhusishwi na kisababishi kingine.


Sambamba na hilo Dkt.Mwendwa amewataka Waandishi wa Habari na Maafisa Habari kuwa Mabalozi wazuri katika kampeni hiyo ya chanjo ya Polio na kutoa Elimu sahihi kwa Wananchi kwa kushirikia na mamlaka husika.



WIZARA YA AFYA KUANZA KUTOA CHANJO YA POLIO YA MATONE. WIZARA YA AFYA  KUANZA KUTOA CHANJO YA POLIO YA MATONE. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on August 20, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.