test

MAZOEZI YAINGEZA HAMASA MANYARA TANZANITE MARATHON

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga, amewataka wananchi wa Mkoa wa Manyara na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kushiriki katika Mbio za Tanzanite Manyara Marathon zinazotarajiwa kufanyika Agosti 22, 2026, wilayani Babati, huku akieleza kuwa ushiriki wao utasaidia kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa watoto njiti.



Mhe. Sendiga ametoa wito huo leo baada ya kushiriki mazoezi ya pamoja na wananchi mkoani Manyara, ambayo ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kujiandaa kushiriki katika mbio hizo.


Kwa mujibu wa taarifa za waandaaji, hadi sasa zaidi ya washiriki 1,500 wamekwishajiandikisha, huku lengo likiwa ni kufikisha washiriki 3,000 kabla ya siku ya mashindano.


Mbio hizo zitahusisha kilomita 5, 10, 21 na 42, 200m Kwa watoto huku washindi katika makundi mbalimbali wakitarajiwa kupata zawadi ikiwemo fedha taslimu na tuzo.


Tanzanite Manyara Marathon inalenga kuchangisha zaidi ya shilingi bilioni 1.5, ambazo zitatumika kuboresha huduma za afya kwa watoto njiti, ikiwemo ujenzi wa jengo la huduma za watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Hanang pamoja na ununuzi wa vifaa tiba.


Mhe. Sendiga amesema ushiriki wa wananchi katika mbio hizo ni zaidi ya kushiriki michezo, bali ni sehemu ya kuchangia jitihada za kuokoa maisha ya watoto wanaohitaji huduma maalumu za afya, huku akiwataka wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana ili kufanikisha lengo hilo.

MAZOEZI YAINGEZA HAMASA MANYARA TANZANITE MARATHON MAZOEZI YAINGEZA HAMASA MANYARA TANZANITE MARATHON Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on August 09, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.