test

AJALI YA LORI YAUA ASKARI NA MAHABUSU SEKENKE ,SINGIDA

  Watu 12 wamefariki na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari la Polisi lililokuwa limewabeba mahabusu na askari kugongwa na lori la mizigo katika eneo la Mlima Sekenke, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.



Gari hilo lilikuwa na watu 13, wakiwamo mahabusu wanane na askari watano, waliokuwa wakisafirisha mahabusu kutoka Kituo cha Polisi Shelui kwenda Mahakama ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi.


Taarifa za awali zinaeleza kuwa lori hilo lililokuwa limebeba mafuta ya dizeli kutoka Dar es Salaam kuelekea Rwanda lilifeli breki wakati likishuka Mlima Sekenke na kuligonga gari la Polisi.


Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, huku majeruhi wakipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Iramba kwa matibabu na taarifa zaidi zikitarajiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida.

#Vision media Tz News Update 

AJALI YA LORI YAUA ASKARI NA MAHABUSU SEKENKE ,SINGIDA AJALI YA LORI YAUA ASKARI NA MAHABUSU SEKENKE ,SINGIDA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 21, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.