test

NAIBU WAZIRI REGINA AKABIDHI PHOTOCOPY, JEZI NA MIPIRA SHULE YA MSINGI BONGA


Naibu Waziri wa Utumishi na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara, *Mhe. Regina Ndege*, amekabidhi *mashine ya Photocopy, jezi na mipira* kwa Shule ya Msingi Bonga.




Msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa maombi ya shule hiyo. Makabidhiano yamefanyika mbele ya Diwani wa Kata ya Bonga, *Mhe. Hitii Khambalali


Mhe. Regina aliambatana na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Manyara *Ndg. Fatuma Tsea*, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Babati Mjini na Diwani wa Viti Maalum *Ndg. Eva Makilagi Luoga*, pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali Kata ya Bonga.


Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Manyara, Ndg. Fatuma Tsea, amempongeza Mhe. Regina kwa majitoleo yake makubwa kwa jamii.


Amesema wanawake hawakukosea kumchagua Mhe. Regina, na kusisitiza kuendelea kumuombea kwa kuwa amefanyika baraka kwa Mkoa wa Manyara kwa kujitahidi kutatua changamoto za Wanamanyara - hasa kwa wagonjwa, walemavu, wasiojiweza, makanisani, misikitini na changamoto mbalimbali za kijamii kadri awezavyo.


Kwa upande wake, Mhe. Regina amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan*, kwa uboreshaji mkubwa wa sekta ya Elimu nchini.


Amesema mabadiliko makubwa yamefanyika mashuleni na kuwawezesha wanafunzi kujifunza katika mazingira mazuri na bora.


Uongozi wa Shule ya Msingi Bonga, walimu na wanafunzi wamemshukuru Mhe. Regina kwa msaada huo muhimu utakao boresha ufundishaji na michezo shuleni.

NAIBU WAZIRI REGINA AKABIDHI PHOTOCOPY, JEZI NA MIPIRA SHULE YA MSINGI BONGA  NAIBU WAZIRI REGINA AKABIDHI PHOTOCOPY, JEZI NA MIPIRA SHULE YA MSINGI BONGA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 21, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.