Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Reuben Kwagilwa
(Samtagwa Mamba Longishu), ametoa muda wa wiki mbili kwa Halmashauri ya Mji wa Babati kwa kushirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Kati (IDBWB), kuanza kuweka mawe yatakayoonesha mpaka wa mita 60 kuzunguka Ziwa Babati.
Kwagilwa ametoa agizo hilo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Manyara kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua eneo hilo na kuhoji sababu za kuchelewa kwa utekelezaji wa zoezi hilo licha ya Serikali kutenga fedha katika mwaka wa fedha 2026/27.
Amesema kuchelewa kwa zoezi hilo kunaashiria uzembe, hasa wakati Nchi ikielekea katika msimu wa mvua za El Niño, huku akiwataka Wataalamu wa Halmashauri na Bodi ya Maji kuwa na mpango unaoeleweka kuhusu idadi, ukubwa, umbali na gharama za mawe yanayohitajika.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
September 18, 2026
Rating:

No comments: