test

ZIARA YA MBUNGE KATA YA NDURUMA TAREHE 16/09/2026.

 

WANANCHI WA KATA YA NDURUMA WAMEJITOKEZA KWA WINGI KUMPOKEA MBUNGE WA JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI MHE. DKT JOHANNES LEMBULUNG LUKUMAY, WAKIELEZA MATUMAINI YAO KUWA UJIO WAKE UTAKUWA SEHEMU YA SULUHISHO LA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOWAKABILI.


Katika ziara hiyo, Mbunge alitembelea Shule ya Sekondari Olemedeye na kukagua maendeleo ya ujenzi wa bweni la wasichana, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza usalama na ustawi wa wanafunzi. Hata hivyo, pamoja na mapokezi hayo. 



WANANCHI WA KATA YA NDURUMA WAFIKISHA KERO ZAO KWA MBUNGE.


KAULI YA MBUNGE BAADA YA KUPOKEA KERO MBALIMBALI ZA WANANCHI WA KATA YA NDURUMA.


Akizungumza baada ya kusikiliza kero hizo, Mbunge alisema ziara yake imelenga kusikiliza wananchi moja kwa moja na kubaini changamoto zinazohitaji hatua za haraka katika Jimbo la Arumeru Magharibi.


Alisema suala la miundombinu, hususan barabara, makorongo na vivuko, haliwezi kutenganishwa na usalama wa wananchi na maendeleo ya shughuli zao za kiuchumi.


Mbunge aliwahakikishia wananchi kuwa kero hizo atazifikisha katika mamlaka husika na kuzifuatilia ili hatua zichukuliwe kwa kuzingatia uhitaji na mazingira halisi ya maeneo hayo.


Akizungumzia changamoto ya mvua, alisisitiza umuhimu wa wataalamu wa halmashauri kutoka ofisini na kufika maeneo yenye changamoto ili kuona hali halisi na kupanga hatua zinazofaa kukabiliana na mafuriko na uharibifu wa miundombinu.


Alisema pia atafuatilia changamoto ya kivuko cha Mto Maroroi pamoja na barabara zinazounganisha vijiji vya Kata ya Nduruma, akisisitiza kuwa miundombinu hiyo ni muhimu kwa wananchi kufikia huduma za kijamii na masoko.


Kwa upande wa elimu, Dkt Lukumay alisema ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Olemedeye ni hatua muhimu katika kuboresha mazingira ya elimu, huku akisisitiza umuhimu wa kukamilisha mradi huo kwa wakati.


Ziara hiyo iliendelea katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Nduruma, huku wananchi wakitumia fursa hiyo kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja kwa mbunge na kuomba ziwe sehemu ya vipaumbele vya maendeleo vya jimbo.

Mbunge Arumeru Magharibi 

#MbungeYupoKazini

#ArumeruMagharibiKwanza

ZIARA YA MBUNGE KATA YA NDURUMA TAREHE 16/09/2026. ZIARA YA MBUNGE KATA YA NDURUMA TAREHE 16/09/2026. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 18, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.