test

RC MANYARA AMKABIDHI MAMA YAKE MTOTO ALIYEPOTEA BAADA YA DNA


Mtoto aliyekuwa ametelekezwa katika kituo kidogo cha mabasi eneo la TANESCO mjini Babati, amepatikana na kukabidhiwa kwa mama yake mzazi baada ya kufanyika kwa vipimo vya DNA.




Mtoto huyo mwenye umri wa miezi minne , aliyekuwa akifahamika awali kwa jina la Baraka Glory Lazaro , amethibitishwa kuwa ni Fadhilieli Ezra Stephano, mkazi wa Kahama, Mkoa wa Shinyanga, baada ya vipimo kufanyika kupitia Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.


Mama mzazi amesema mtoto huyo alipotea katika eneo la soko alipomwacha kwa muda wakati akienda kufanya shughuli zake. Aliporejea alimkuta hayupo na juhudi za kumtafuta hazikuzaa matunda.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Martine Shigela, amewashukuru wataalamu na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kusaidia kuthibitisha uhusiano wa mtoto huyo na mama yake, pamoja na Glory Lazaro kwa kumlea mtoto wakati akisubiri familia yake kupatikana.


Shigela ametoa wito kwa jamii kushirikiana katika ulinzi na malezi ya watoto, huku akiwataka wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapokutana na watoto waliopotea au walio katika mazingira hatarishi.

RC MANYARA AMKABIDHI MAMA YAKE MTOTO ALIYEPOTEA BAADA YA DNA  RC MANYARA AMKABIDHI MAMA YAKE MTOTO ALIYEPOTEA BAADA YA DNA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 16, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.