test

RC SHIGELA AHIMIZA MSHIKAMANO KWA VIONGOZI NA WATUMISHI BABATI DC

 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, *Mhe. Martine Reuben Shigela*, leo amefanya ziara ya kujitambulisha katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati.




Katika ziara hiyo, Mhe. Shigela ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa ushirikiano wao mzuri unaoifanya Halmashauri kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.


Aidha, Mhe. Shigela amewahimiza viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Vijijini kuwa na mshikamano na kufanya kazi kama timu moja.





Mhe. Shigela amewataka Madiwani na watumishi kuacha ubinafsi na kufanya kazi kwa pamoja ili wananchi wafaidike na maendeleo yaliyokusudiwa na Serikali ya Awamu ya Sita.


Vilevile, amewaasa viongozi kuondoa matabaka katika uongozi na kusisitiza uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.


Mhe. Shigela ameahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wote ili kuendelea kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Manyara.

RC SHIGELA AHIMIZA MSHIKAMANO KWA VIONGOZI NA WATUMISHI BABATI DC RC SHIGELA AHIMIZA MSHIKAMANO KWA VIONGOZI NA WATUMISHI  BABATI DC Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 25, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.