test

RC SHIGELA AHIMIZA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI NA WATUMISHI WA UMMA BABATI MJINI


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Martine Reuben Shigela, leo Septemba 25, 2026, ameendelea na ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Mji wa Babati.



Katika ziara hiyo, Mhe. Shigela amekutana na kufanya kikao na viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, ambapo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika utendaji kazi.

Mhe. Shigela amesema, ili adhma ya Serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo ifanikiwe, ni lazima viongozi na watumishi washirikiane, wawe na umoja na kufanya kazi kama timu moja.





Ameongeza kuwa, hakuna Halmashauri itakayopiga hatua ya maendeleo kama kila mmoja atafanya kazi kwa kujitenga, bali maendeleo ya kweli yanatokana na mshikamano, uwajibikaji na kuzingatia maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
RC SHIGELA AHIMIZA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI NA WATUMISHI WA UMMA BABATI MJINI RC SHIGELA AHIMIZA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI NA WATUMISHI WA UMMA BABATI MJINI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 25, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.