Septemba 24, 2026 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Martine Shigela, amewataka viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' kushirikiana kwa karibu katika kutekeleza shughuli za maendeleo na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinawanufaisha wananchi.
Akizungumza katika kikao na viongozi pamoja na watumishi wa Halmashauri hiyo, Mhe. Shigela amesisitiza umuhimu wa kila kiongozi kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya kazi, uwajibikaji, uadilifu na utu, sambamba na utekelezaji wa vipaumbele vya Serikali.
Mhe. Shigela pia amewataka viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo kuongeza juhudi katika kukusanya mapato ya Halmashauri, akieleza kuwa mapato ni sehemu muhimu ya kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi.
Aidha, amewataka viongozi kuwa karibu na wananchi, kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili na kuzifanyia kazi kwa wakati, ili kujenga imani na ushirikiano kati ya Seri
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
September 24, 2026
Rating:

No comments: