test

SILLO,AMUOMBA RC SHIGELA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARIDHI

 


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, *Mhe. Daniel Sillo*, leo amemkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Martine Reuben Shigela, aliyefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati (Babati DC).



Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Sillo ameahidi kumpa ushirikiano wa dhati Mkuu wa Mkoa katika kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi wa Manyara maendeleo.




Mhe. Sillo ameeleza kuwa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati lina ushirikiano mkubwa, jambo linalorahisisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.





Aidha, Mhe. Sillo amemuomba Mkuu wa Mkoa kushughulikia mgogoro wa ardhi katika Halmashauri hiyo, hususani katika Kata ya Kiru, ambapo kumekuwa na migogoro ya ardhi isiyoisha kwa muda mrefu.



Vilevile, Mhe. Sillo ameeleza changamoto ya bei ya mazao kuwa chini huku pembejeo zikiwa na gharama kubwa, hali inayowaathiri wakulima wa Babati Vijijini.




Akijibu Changamoto hizo mhe Mkuu wa Mkoa WA Manyara mhe.Martine Shigela ameeleza kuwa yupo tayari kushughulika na masuala yaliyo elezwa husani migogoro ya Aridhi kwakushirikiana na wadau wote, ikiwemo migogoro ya Aridhi baina ya Wananchi na wawekezaji.



Shigela amesema kuwa ili kujengsma mshikamano na USHIRIKIANO katika jamii ni vyema migogoro baina ya wawekezaji na Wananchi itatuliwe ili kuwe na usawa katika jamii na kuwa na UWEKEZAJI wenye tija pasipo kuhitilafiana.

SILLO,AMUOMBA RC SHIGELA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARIDHI SILLO,AMUOMBA RC SHIGELA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARIDHI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 25, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.