test

TPDC YAFIKISHA GESI ASILIA MAJUMBANI KATIKA MIKOA MINNE

 

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limefanikiwa kusambaza gesi asilia kwa matumizi ya majumbani katika mikoa minne nchini, ambayo ni Lindi, Mtwara, Pwani na Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza matumizi ya nishati safi na salama kwa wananchi.



Hayo yamesemwa na Mhandisi wa TPDC Hassan Temba wakati akitoa semina ya kuongeza uelewa kwa wanahabari mkoa wa Manyara juu ya shirika hilo lakini pia kueleza kuhusu muendelezo wa utekelezaji wa bomba la mafuta ghafi kutoka Goima nchini Uganda hadi chongoliani mkoani Tanga nchini Tanzania.


Amesema pia kuwa matumizi ya gesi asilia majumbani yanaendelea kupewa kipaumbele kutokana na umuhimu wake katika kupunguza utegemezi wa nishati nyingine na kuboresha mazingira ambapo hadi sasa jumla ya nyumba 2500 zimekwisha unganishwa na huduma ya nishatibya gesi kwaajili ya matumizi manyumbani.


Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa TPDC, Francis, amesema zaidi ya visima 96 vimechimbwa hadi sasa katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia, hatua inayolenga kuongeza usambazaji wa nishati hiyo kufika maeneo mengi zaidi na watumiaji wengi ili kuongeza tija ya uwepo wake hapa nchini.




Kwa sasa TPDc inaeleza  utafiti wa mafuta na gesi asilia ni sehemu ya miradi ya kimkakati ya Taifa, inayolenga kubaini na kuendeleza rasilimali za petroli ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuongeza upatikanaji wa nishati ya gesi na mafuta huku ikilenga pia kuuza katika maeneo ya nchi za jirani ikiwemo zambia,kenya malawi na nyinginezo.





TPDC YAFIKISHA GESI ASILIA MAJUMBANI KATIKA MIKOA MINNE TPDC YAFIKISHA GESI ASILIA MAJUMBANI KATIKA MIKOA MINNE Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 10, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.