test

WALINZI WANNE WA KAMPUNI YA QWIHAYA MBARONI KWA MAUAJI

 Walinzi wanne wa kampuni ya Qwihaya wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Njombe kwa tuhuma za kumuua Joseph Mwenda (33), baada ya kumtuhumu kuwa alikuwa akiiba magogo waliyokuwa wakilinda.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Septemba 18, 2026, huku mwili wa Mwenda ukibainika Septemba 20, saa 10 jioni, ukiwa umefichwa kichakani.


Amesema uchunguzi wa awali umebaini marehemu alishambuliwa katika sehemu mbalimbali za mwili kabla ya kufichwa kichakani. Watuhumiwa hao, ambao ni walinzi wa Suma JKT, wanadaiwa kumshambulia baada ya kumtuhumu kuhusika na wizi wa magogo katika eneo walilokuwa wakilinda, Mtwango wilayani Njombe.


“Watu wanne wanashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo la mauaji,” amesema Banga.


Kamanda Banga amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi, akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kosa na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.


Jirani wa marehemu, Samson Mgaya, amesema amesikitishwa na tukio hilo na kuiomba Polisi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa ili kuzuia matukio

WALINZI WANNE WA KAMPUNI YA QWIHAYA MBARONI KWA MAUAJI WALINZI WANNE WA KAMPUNI YA QWIHAYA MBARONI KWA MAUAJI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 22, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.