Wananchi Wa Kata ya Dabili wilayani Babati mkoani Manyara, wameanza RASMI uchimbaji wa MSINGI wa majengo ya madarasa, kwaajili ya MAANDALIZI ya kupokea wanafunzi wa kidato Cha kwanza Mwaka 2028.
Akizungumza wakati wa zoezi la uchimbaji wa MSINGI wa madarasa 3 na ofisi 1 katika SHULE ya SEKONDARI Maganjwa, DIWANI wa Kata ya Dabil Mhe leonce Gwandu, amesema madarasa hayo yataanza KUJENGWA Kwa ufadhili wa shirika la KARIMU FOUNDATION, ambapo Kwa Sasa wameanza kuchimba MSINGI SEKONDARI ya Maganjwa na SEKONDARI ya Dabil ambapo Kila SHULE wameanza na MSINGI wa madarasa 3 na ofisi.
Aidha mhe Gwandu amewashukuru wa fadhili wa KARIMU FOUNDATION Na kuahidi kuwapa USHIRIKIANO wa kutosha ili kutimiza Azma ya maendeleo katika Kata hiyo.
Nao Wananchi Wa Kata hiyo wameshukuru Kwa madarasa hayo, na kuiomba KARIMU FOUNDATION,kuwasaidia katika Kuwasaidia kwenye MIRADI ya maji na uboreshaji wa MIUNDO mbinu katika Kata hiyo.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
October 10, 2026
Rating:




No comments: