Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Johanes Stephen Kerya, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Mkoa wa Singida, na kumteua kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) Manyara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Oktoba 14, 2026, Kerya anachukua nafasi hiyo baada ya uhamisho huo wa kikazi.
Katika mabadiliko hayo, Kamanda Kerya anachukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACP) Makarani Khamis Ahamed, ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kukabiliana na Dharura, Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Mabadiliko hayo yametangazwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, kupitia taarifa iliyotolewa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
MAKARANI AHAMISHIWA MAKAO MAKUU YA POLISI DODOMA
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
October 14, 2026
Rating:
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
October 14, 2026
Rating:

No comments: