test

AJALI YA GARI ENDULENI YAGHARIMU MAISHA YA WATU WATATU, SABA WAJERUHIWA

 


Watu watatu wamefariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya Land Rover yenye namba za usajili T 227 AZJ iliyotokea Novemba 9, 2026, majira ya saa 10:00 jioni katika eneo la Esirwa, Kijiji na Kata ya Endulen, Wilaya ya Ngorongoro.



Taarifa za awali zinaeleza kuwa gari hilo lilikuwa likitokea Karatu kuelekea Endulen kabla ya kupata hitilafu katika mfumo wa breki na kupinduka, na kusababisha vifo vya watu watatu ambao ni wanaume wawili na mwanamke mmoja.



Aidha, watu saba wamejeruhiwa katika ajali hiyo, wakiwemo wanaume wanne, wanawake wawili na mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.


Majeruhi wote walikimbizwa katika Hospitali ya Endulen kwa ajili ya matibabu,  wakiendelea kupatiwa matibabu. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.


Akitoa pole kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mhe. Lt. Col. Robert Augustino Kakomangile, ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu waliopoteza wapendwa wao, huku akiwatakia majeruhi wote nafuu ya haraka.


Mkuu wa Wilaya  amesisitiza umuhimu wa kuzingatia usalama barabarani na kuhakikisha vyombo vya usafiri vinakaguliwa mara kwa mara ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa ajali zinazoweza kuepukika

AJALI YA GARI ENDULENI YAGHARIMU MAISHA YA WATU WATATU, SABA WAJERUHIWA AJALI YA GARI ENDULENI YAGHARIMU MAISHA YA WATU WATATU, SABA WAJERUHIWA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on November 09, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.