Watu 21 wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria aina ya Maokoto Express lililogongana na lori la mizigo katika eneo la Masumbo, njiapanda ya Kiponzelo, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, kwenye barabara kuu ya TANZAM (Iringa–Mbeya).
Kwa mujibu wa mashuhuda, basi hilo lilikuwa likitoka Kijiji cha Wasa, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, kuelekea Iringa Mjini kabla ya kupata ajali hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, imeeleza kuwa watu 21 wamepoteza maisha, wakiwemo wanaume 10, wanawake tisa na watoto wawili, huku wengine watano wakijeruhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, chanzo cha awali cha ajali kinadaiwa kuwa ni hitilafu katika mfumo wa breki wa basi hilo, iliyosababisha dereva kushindwa kulidhibiti. Basi hilo liliingia barabarani kwa kasi na kugongana na lori la mizigo.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
November 09, 2026
Rating:

No comments: