test

ALIYEKUWA MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI DAR ES SALAAM MARISON MWAKYOMA ASIMIKWA RASMI KUWA MCHUNGAJI

 

Aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (Zonal Traffic Officer – ZTO) Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Marison Mwakyoma, ameamua kuendeleza utumishi wake kwa kumtumikia Mungu kupitia huduma ya kuhubiri Injili baada ya kustaafu utumishi wa Serikali.



Mwakyoma, ambaye awali alihudumu katika nafasi ya Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, sasa amejiunga na huduma ya kichungaji katika Kanisa la Evangelical Brotherhood, lililopo chini ya uongozi wa Askofu Dkt. Rabson Mwakanani Mambya, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Evangelical Brotherhood Tanzania.


Katika hatua hiyo, tarehe 8 Novemba 2026, Marison Mwakyoma amesimikwa rasmi kuwa Mchungaji katika kanisa hilo, hatua inayotajwa kuwa mwanzo wa safari mpya ya kulitumikia kanisa na kueneza Neno la Mungu.


Uamuzi huo ni mfano wa namna mtu anavyoweza kuendelea kulitumikia taifa na jamii kwa njia tofauti, huku akijitoa katika kazi ya Mungu kupitia huduma ya kiroho.


Kusimikwa kwa Mchungaji Marison Mwakyoma ni habari njema kwa Kanisa la Mungu nchini Tanzania na duniani kote, huku akitakiwa kuwa mwaminifu katika wito na wajibu mpya aliopewa wa kuhubiri Injili na kuliongoza kundi la Mungu.

ALIYEKUWA MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI DAR ES SALAAM MARISON MWAKYOMA ASIMIKWA RASMI KUWA MCHUNGAJI ALIYEKUWA MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI DAR ES SALAAM MARISON MWAKYOMA ASIMIKWA RASMI KUWA MCHUNGAJI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on November 09, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.