NAIBU WAZIRI REGINA NDEGE ASHIRIKI IBADA YA KIPAIMARA MAGUGU - ATOA MIFUKO 200 YA SARUJI KWA UJENZI WA KANISA
Naibu Waziri Utumishi na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara, *Mhe. Regina Ndege* Nov 8, 2026 ameshiriki Ibada ya Kipaimara Parokia ya Magugu iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo la Mbulu, *Mhashamu Anthony Lagwen*.
Aidha katika ibada hiyo ilifanyika Harambee ya ujenzi wa Kanisa hilo ambapo zilipatikana *fedha taslimu kiasi zaidi ya Tsh Milioni 12*, huku Mhe. Regina akitoa *Mifuko 200 ya Saruji*
Mhe. Regina aliliomba Kanisa kuliombea Taifa, kudumisha amani, umoja na mshikamano.
Mhe. Regina aliambatana na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Manyara, *Ndg. Fatuma Tsea*, Diwani wa Kata ya Magugu, *Mhe. Stanley Dismas* na Diwani wa Viti Maalum, *Mhe. Stahimili Masasi*.
NAIBU WAZIRI REGINA NDEGE ASHIRIKI IBADA YA KIPAIMARA MAGUGU - ATOA MIFUKO 200 YA SARUJI KWA UJENZI WA KANISA
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
November 08, 2026
Rating:
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
November 08, 2026
Rating:



No comments: