JUMLA YA MIL 19.1, ZA DAIWA KWA VIKUNDI VILIVYOKOPA HALMASHAURI YA WILAYA YA BABATI, BARAZA LA MADIWANI WATOA MAADHIMIO.
Suala la Mikopo inayotolewa na halmashauri kwa vijana kina mama na walemavu laibua mjadala mzito,katika Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Babati kutokana na kucheleweshwa kwa marejesho.
Hayo yameibuka Leo Novemba 10.2026 katika kikao Cha Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo Cha Robo ya kwanza julai September 2026-2027.
Akifungua kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo mhe John Noya amebainisha Kata ambazo Zina daiwa fedha nyingi na kupelekea Kata hizo kupewa adhabu kufungiwa kupewa mikopo Mpaka kurejesha fedha wanazo daiwa.
Miongoni mwa Kata zenye vikundi sugu ni Pamoja na Galapo secheda, huku Kata zingine zikiwa Zina daiwa kiasi kidogo.
Wakichangia suala hili baadhi ya madiwani wameshauri Kata zenye kudaiwa madeni sugu VIKUNDI vichukuliwe hatua za kisheria ili fedha hizo ziweze kurejeshwa katika halmashauri.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
November 10, 2026
Rating:



No comments: