Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, anatarajiwa kufikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo Novemba 19, 2026, kwa ajili ya kutajwa kwa kesi nyingine ya makosa ya mtandaoni inayomkabili.
Lissu anakabiliwa na mashtaka matatu yanayohusiana na madai ya kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa YouTube, akidaiwa kutoa kauli hizo Aprili 3, 2025. Kauli hizo zinahusu kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, matumizi ya polisi katika masuala ya uchaguzi na madai ya baadhi ya majaji kutokuwa na upendeleo.
Kesi hiyo inatajwa siku 13 baada ya Mahakama Kuu kumwachia huru Lissu dhidi ya shtaka la uhaini, lakini kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi na kumhukumu kifungo cha miaka minne jela, Novemba 6, 2026.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
November 18, 2026
Rating:

No comments: