test

KESI YA PAMBALU KUAJWA KESHO KISUTU.

 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa kesi ya uhaini inayomkabili Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uchaguzi wa chama hicho, John Pambalu, itatajwa kesho Novemba 18, 2026, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 17 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, kesi hiyo itatajwa mbele ya Hakimu Mashasha saa 3:00 asubuhi.


CHADEMA imetoa wito kwa viongozi, wanachama, wadau wa haki na demokrasia pamoja na wananchi kufika mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.


Chama hicho kimesema wito huo ni sehemu ya kuendeleza utaratibu wa kushiriki mashauri mbalimbali yanayogusa haki na misingi ya demokrasia nchini.

KESI YA PAMBALU KUAJWA KESHO KISUTU. KESI YA PAMBALU KUAJWA KESHO KISUTU. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on November 17, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.