test

DC BABATI NA DED WAWAPONGEZA WADAU WA MAENDELEO



 Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela  Kaganda  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo wamepongeza Wadau wa maendeleo walioko katika H/ Wilaya ya Babati kwa kushirikiana na Serikali katika kuwaletea Wananchi maendeleo . Viongozi hao wameyasema hayo leo kwenye  Kikao maalum cha kamati ya ushauri  ya Wilaya (DCC)  cha kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya kwa mwaka 2026/2027 kilichofanyika katika   katika Ukumbi wa Halmashauri ambapo Halmashauri Wilaya ya Babati. TARURA, RUWASA , BAWASA , Shirika  Karimu Foundati na So They Can  (STC) wamewasilsha mipango na Bajet zao. "Tunawashukuru sana wadau wote wa maendeleo  katika Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na Serikali kuwaletea  Wananchi  maendeleo wamesisitiza viongozi hao. Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo ameomba wadau hao kuweka mpango wa kujenga Madarasa  ya kidato cha kwanza kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi Kwa  mwaka 2028 ambapo wanafunzi walipo sasa darasa la Sita  na walioko darasa la Tano mwaka huu  wote kwa pamoja watakutana Kidato Cha kwanza mwaka 2028.


 

Wakati huo  huo Mhe. Kaganda amesisitiza TARURA wanapotengeneza Barabara kuhakikisha wanatengeneza mitaro ya maji na kushughulikia maeneo yote korofi kwenye Barabara.

Kwa upande wa RUWASA na BAWASA , Mhe Kaganda amewasisitiza   wanapojenga miradi ya maji wahakikishe  maji yanafikishwa kwenye Taasisi  Umma mf shule  hospital na vituo vya Afya.. Kikao Cha kamati ya Ushauri  Wilaya  kimehudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Vyama vya siasa, Watendaji na wataalamu Kutoka Taasisi , Idara na wakala wa Serikali zilizomo katika Hamshauri ya Wilaya ya Babati.

DC BABATI NA DED WAWAPONGEZA WADAU WA MAENDELEO DC BABATI NA DED WAWAPONGEZA WADAU WA MAENDELEO Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on February 07, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.