test

MADIWANI BABATI DC WALALAMIKIA WATENDAJI WA VIJIJI

 


Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wamelalamikia Suala la Utovu wa nidhamu Kwa baadhi ya watendaji wa VIJIJI katika Halmashauri hiyo, Jambo linalopelekea kudorora Kwa Maendeleo ya Kata.



Madiwani hao wameeleza hayo katika KIKAO Cha Baraza la MADIWANI Cha Robo Ya 3 ya Mwaka kilichoketi Aprili 29.2026.

Baadhi ya Mambo yaliyolalamikiwa Kwa watendaji hao ni Pamoja na Ubadhirifu wa Mali za Umma, Uzembe, Utoro pamoja na Ulevi.

Miongoni mwa VIJIJI vilivyolalamikiwa Zaidi ni pamoja na Ufana,Kata ya Ufana,Aya mango Kata ya Galapo na VIJIJI vingine.

Mwenyekiti Wa Halmashauri Hiyo Mhe.John Noya amekiri kuwepo Kwa Tatizo Hilo na kumuagiza mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo kuochukua Hatua Zinazo staili Kwa watendaji hao ili kuzinusuru Kata hizo na matatizo ya hapa na pale ikiwemo malalamiko mengi ya Wananchi.



Akijibu tuhuma hizo Mbele ya MADIWANI Hao Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Bw.John Ntabagi ambaye ni Afisa utumishi wa halmashauri Hiyo Amesema Matatizo hayo wanayafahamu na wameshachukua Hatua Kwa Baadhi ya watendaji WALIO Bainika na makosa hayo na kuwa Bado wanaendelea kushughulikia Watendaji wengine ambao wanaonekana Wana Matatizo yanayolalamikiwa na MADIWANI.

MADIWANI BABATI DC WALALAMIKIA WATENDAJI WA VIJIJI MADIWANI BABATI DC WALALAMIKIA WATENDAJI WA VIJIJI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on April 29, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.