test

GARI LILOKUWA LIMEBEBA NA WANA HABARI LA PATA AJALI SHINYANGA.

 Gari lililokuwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga limepata ajali katika eneo la Usanda, wilayani Shinyanga, kwenye barabara kuu ya Tabora–Shinyanga.



Kwa mujibu wa taarifa za awali, ajali hiyo ilitokea baada ya gari hilo kujaribu kukwepa gari aina ya Toyota Harrier kabla ya kupoteza mwelekeo na kuingia mtaroni.


Watu watano wamejeruhiwa katika ajali hiyo, akiwemo Mwandishi wa Habari wa ITV/Radio One,Frank Mshana, pamoja na Johnson Zacharia na Boazi.


Majeruhi wote wamewahishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


Taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo na hali za majeruhi zinatarajiwa kutolewa kadri zitakavyokuwa zinapatikana.

GARI LILOKUWA LIMEBEBA NA WANA HABARI LA PATA AJALI SHINYANGA. GARI LILOKUWA LIMEBEBA NA WANA HABARI LA PATA AJALI SHINYANGA. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on May 19, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.