test

SILLO AONGOZA JOGGING MWADA,ASISITIZA UMOJA NA UZALENDO.*


Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daniel Sillo, ameshiriki zoezi la jogging katika Kata ya Mwada wilayani Babati, mkoani Manyara, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha afya, maendeleo, uzalendo na ushirikiano katika jamii.



Katika shughuli hiyo iliyoambatana na uzinduzi wa jezi mpya za Mwada Jogging Club, Mheshimiwa Sillo amekubali kuwa mwanachama na mlezi wa klabu hiyo, pamoja na kuahidi kusaidia upatikanaji wa jezi kwa ajili ya wanachama na kuwapatia redio itakayosaidia katika mazoezi yao.


Sillo amesema kuwa afya ni msingi wa maisha na maendeleo, akisisitiza kuwa jamii yenye afya ina uwezo mkubwa wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kijamii.




"Afya ni uchumi, afya ndiyo maisha. Tunapaswa kuendelea kushirikiana kuimarisha afya zetu na kujenga jamii yenye nguvu," amesema Sillo.


Wakizungumza wakati wa hafla hiyo, viongozi wa Mwada Jogging Club wameeleza kuwa klabu hiyo imeendelea kukua na hadi sasa ina wanachama 64 wanaoshiriki mazoezi kwa ratiba maalum ya kila Jumanne, Alhamisi na Jumamosi.


Katibu wa Mwada Jogging Club, Rajabu Shabani, amesema wanachama wa klabu hiyo wameamua kumuomba Mheshimiwa Sillo kuwa mlezi wao kutokana na mchango wake katika kuhamasisha maendeleo na ushirikiano katika jamii.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mwada Jogging Club, Laurent Mokeva, amesema jogging imekuwa na mchango mkubwa kwa wanachama kwani mbali na kuimarisha afya, imewasaidia pia kupata marafiki wapya na kujenga mahusiano mazuri katika jamii.


Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Babati, Mrakibu wa Polisi (SP) Ernesta Mwambinga, amesema vikundi vya jogging vina nafasi kubwa katika kuimarisha uzalendo, amani na mshikamano miongoni mwa wananchi.


Amesema ushiriki wa wananchi katika michezo na mazoezi ni njia mojawapo ya kujenga jamii yenye afya bora na mahusiano mazuri.



SILLO AONGOZA JOGGING MWADA,ASISITIZA UMOJA NA UZALENDO.* SILLO AONGOZA JOGGING MWADA,ASISITIZA UMOJA NA UZALENDO.* Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on June 13, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.