JUBILEE YA MIAKA 25 MAMIRE: NAIBU WAZIRI REGINA ACHANGISHA MILIONI 7.4, ATOA WITO WA KULIIOMBEA TAIFA NA RAIS SAMIA
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara, Mhe. Regina Ndege, Jumapili ya Julai 26, 2026 ameshiriki maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 25 ya Kwaya ya Mtakatifu Karoli Lwanga Parokia ya Mamire, Wilaya ya Babati.
Mhe. Regina aliambatana na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Manyara, Ndg. Fatuma Tsea, Madiwani wa Viti Maalum wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Diwani wa Kata ya Mamire.
Akumbusha umuhimu wa kuliombea Taifa
Akizungumza na waumini katika misa ya shukrani, Mhe. Regina alikumbusha kanisa kuhusu wajibu wake wa kuliombea Taifa na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,ili Mungu azidi kumpa nguvu na hekima katika kuongoza nchi.
Katika maadhimisho hayo, kwaya ilikuwa na lengo la kukusanya Tsh. milioni 6 kwa ajili ya kurekodi audio na video ya nyimbo zao.
Mhe. Regina aliongoza zoezi la uchangishaji na kuchangia mwenyewe Tsh. 1,500,000/= Kwa pamoja kiasi cha Tsh. 7,482,600/= kilipatikana, huku fedha taslimu iliyopokelewa ikiwa Tsh. 6,565,600/= na ahadi Tsh. 917,400/=.Hivyo lengo lilivukwa
Ahadi ya mifuko 100 ya saruji kwa daraja la Mwikansi
Pia katika hafla hiyo, Mhe. Regina alitoa ahadi ya mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mwikansi.
Akitumia fursa hiyo, Diwani wa Kata ya Mamire aliomba msaada wa ujenzi huo. Amesema jamii imeshachukua hatua kwa kuchangia mawe na mchanga pamoja na kiasi cha Tsh. milioni 5.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
July 26, 2026
Rating:










No comments: